31 August 2010
Baba,Mama na Mtoto wakiwa katika pikipiki yao kwa staili ya kichina china,sasa sijui inakuwaje katika swala zima la kiusalama.maana huyo dereva anaonekana ni mwanafunzi kutokana na hiyo alama hapo nyuma,pili hicho kiti hapo nyuma kilichokaliwa na mtoto,tatu wao wazazi wamevaa kofia za kiusalama na mtoto amepozi kimpango wake.daah hii kweli bongo daslam
30 August 2010
Wakazi wa jijini wakiangalia gari namba T 729 BFD aina ya Fiati likiwa lililopinduka baada ya kugongana na gari lingine aina ya Fuso lililokuwa limebeba nyanya katika makutano ya barabara ya Morogoro na ile inayotoka Sinza maeneo ya shekilango Dar es Salaam asubuhi leo. Katika ajali hiyo dereva wa fuso na kondakta wake walifariki papo hapo na wale waliokuwepo katika Fiati wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili
Subscribe to:
Posts (Atom)