21 September 2010

"WAGONJWA KATIKA VITANDA VYA KAMBA HUPOTEZA MATUMAINI YA KUPONA"


Jamani watu tulio mijini tusilalamike saaan kuhusu huduma za Hospitali zetu kwani tunaweza kumkufuru Mungu kwa hata kidogo tulichojaaliwa, kwani kuna wenzetu katika baadhi ya Vijiji vya nchini kwetu humu humu hawapati hata kile kidogo ambacho kinawezakupatikana katika hospitali nyingine. Na pia katika baadhi ya sehemu kumekuwa na malalamiko ya watu kuhusu upungufu wa madawa, huduma na hata upungufu wa vitanda ambapo wengine huweza kulazwa wagonjwa 2 hadi 4 katika kitanda kimoja. Mbali na hayo yote Mdau hebu anagalia picha hii hawa ni wagonjwa katika mkoa fulani, wakiwa wamelazwa wodini na tena wakiwa wamewekewa Drip, eti kitanda chenyewe ni cha kamba je ungelikuwa wewe Mdau ungejisikiaje na je ukienda katika hospitali zetu na kupata huduma pungufu lakini inayoridhisha ukilinganisha na hii uliyoiona katika Ukurasa huu utaweza kulalamika?

No comments:

Post a Comment